Utayarishaji Wa Kitalu Bora Cha Mboga Mboga Kuhamisha -Books Pdf

UTAYARISHAJI WA KITALU BORA CHA MBOGA MBOGA KUHAMISHA
26 Mar 2020 | 108 views | 0 downloads | 21 Pages | 288.66 KB

Share Pdf : Utayarishaji Wa Kitalu Bora Cha Mboga Mboga Kuhamisha

Download and Preview : Utayarishaji Wa Kitalu Bora Cha Mboga Mboga Kuhamisha


Report CopyRight/DMCA Form For : Utayarishaji Wa Kitalu Bora Cha Mboga Mboga KuhamishaTranscription

Kilimo bora cha mbogamboga,1 Utangulizi,2 Kitalu ni nini. 3 Sifa za sehemu nzuri ya kutengeneza kitalu,4 Aina au mbinu za uzalishaji za vitalu. 5 Namna ya kuandaa mchanganyiko unaotumika kwenye viriba au boksi. 6 Faida za vitalu vya viriba au trei,7 Vitalu vya matuta. 8 Kutayarisha matuta na mahitaji, 9 Utaratibu wa kupata mbegu za kusia kwenye kitalu. 10 Kusia mbegu,11 Matunzo ya kitalu, 12 Maandalizi ya shamba la ngogwe nyanya na upandaji.
13 Maandalizi ya shamba la mnavu na upandaji, 14 Mambo ya kuzingatia katika utunzaji wa mimea shambani. 15 Uvunaji na uhifadhi wa mboga na matunda,16 Hitimisho. Kilimo bora cha mbogamboga,UTANGULIZI, Mboga za majani ni sehemu muhimu katika mlo wa mwanadamu Mboga hizi hutoa virutubisho. muhimu kama vile protini vitamini na madini ambavyo ni muhimu katika mwili wa mwanadamu. kwa afya bora Ulaji wa mbogamboga katika nchi nyingi za Afrika zilizo chini ya jangwa la. sahara ikiwemo Tanzania upo chini ya kiwango kinachoshauriwa na shirika la chakula la umoja. wa mataifa FAO Hivyo basi uzalishaji wa miche bora kitaluni na utunzaji wa miche. bustanini shambani kwa kutumia mbinu za kisasa ni msingi muhimu sana katika kuboresha. upatikanaji na ulaji wa mboga kwa kaya na jamii kwa jumla. 1 KITALU CHA MBOGA,Kitalu ni nini, Kitalu ni sehemu maalumu iliyopangiliwa kwa ajili ya kutunzia miche michanga kabla ya. kuipeleka shambani ama bustanini Sio mimea yote inahitaji vitalu ila mimea mingi inahitaji. vitalu Mimea kama mahindi maharage karoti kunde na mchicha haihitaji vitalu Mimea kama. kabeji vitunguu sukuma wiki chainizi nyanya bilinganya hoho matikiti matango na. mengineyo huhitaji kitalu Pia miti mingi ya aina mbalimbali kadhalika huhitaji kitalu. Mimea ambayo inasumbua kupandikiza na ambayo inachipua haraka inashauriwa kupandwa. moja kwa moja shambani ambapo haitasumbuliwa kuhamishwa Mimea ambayo inachelewa. kuchipua kukua na yenye kuhitaji matunzo au kuhudumiwa kwa karibu wakati ikiwa michanga. inashauriwa ipandwe kwanza kwenye kitalu hadi itakapopata miche inayotakiwa kisha. kupandikizwa bustanini au shambani,Sifa za sehemu nzuri ya kutengeneza kitalu.
1 Karibu na chanzo cha maji au bomba, 2 Sio mbali na shambani bustanini ambapo miche itahamishiwa. 3 Mbali na wanyama ama kuwe na uzio,4 Pasiwe na upepo mkali. 5 Pasiwe mahali ambapo zao lililooteshwa kabla ni la jamii moja. 6 Iwe na kivuli, 7 Iwe karibu na njia kurahisisha usafirishaji pindi ikibidi. Aina au mbinu za uzalishaji za vitalu,1 Vitalu vya kawaida vya matuta. 2 Vitalu vya mifuko viriba,Kilimo bora cha mbogamboga.
3 Vitalu vya boksi masanduku au trei, Uchaguzi wa mbinu au aina za vitalu hutegemea na uwezo wa mkulima gharama na aina za. mbegu zinazotarajiwa kuoteshwa na upatikanaji wa pembejeo husika. Namna ya kuandaa mchanganyiko unaotumika kwenye vitalu vya viriba au trei au boksi. Kama udongo wa msituni unapatikana uchekechwe kuondoa takataka na mabonge makubwa. Udongo huu unaweza kutumika kwenye viriba kama ulivyo bila kuongeza kitu chochote kwani. huu una rutuba ya kutosha na pia hauna vimelea vya magonjwa. Kutibu udongo wa kwenye viriba, Kama udongo unaotumika ni wa sehemu ambayo imeshatumika kwa mazao mengine basi. chukua udongo wa tabaka la juu debe tano au kipimo chochote mfano kopo au sado kulingana. na kiasi cha udongo unachohitaji mbolea debe sado kopo na makapi ya mpunga ama mchanga. debe sado kopo moja 5 3 1 Mchanganyiko huu uchekechwe kuondoa mabonge makubwa na. takataka ili miche iote vizuri Mchanganyiko huu unaweza pia kupashwa moto kwa dakika 20 30. huku ukiukoroga ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu Kujua kama vimelea vimekufa. wakati wa kupika huo udongo weka kiazi mhogo gimbi katikati ya udongo na hakikisha kila. unapokoroga kiazi kinafunikwa na udongo Baada ya dakika 20 30 angalia kama kiazi au. mhogo umeiva basi udongo uko tayari Acha upoe kwa siku 2 3 kabla ya kuanza kuutumia. Changanya vizuri kwa kutumia koleo na uunyweshee kidogo ili ushikane kabla ya kuanza. kujaza kwenye viriba kuzuia usimwagike Trei zipangwe kwenye kichanja na sio kwenye ardhi. moja kwa moja Panda mbegu mbili kwenye kila tundu na baadaye upunguzie na kuacha mche. mmoja baada ya kuota Baada ya kusia mbegu funika na majani makavu na mwagilia maji kwa. utaratibu kuzuia magojwa ya kitalu Ondoa majani baada ya mbegu kuota na uweke kivuli cha. kiasi juu ya kitalu kuzuia jua na mvua kubwa Kagua kila siku kama kuna ugojwa au wadudu. Faida za vitalu vya viriba au trei,Miche huota vizuri kwa asilimia mia. Ni rahisi kuhamisha vitalu hivi kutoka sehemu moja kwenda nyingine pale linapotokea. tatizo kama wanyama waharibifu au mvua kubwa nk,Unajua idadi ya miche uliyo nayo kwa urahisi. Unaweza kuhamisha miche hii wakati wowote wa hali ya hewa. Kilimo bora cha mbogamboga,Vitalu vya matuta, Kuna matuta ya aina mbili ambayo ni ya makingo na matuta ya kunyanyua au ya meza Aina.
hizi za matuta hutegemea aina ya udongo na kipindi au majira ya mwaka Kwenye udongo wa. mfinyanzi au kipindi cha mvua nyingi matuta yanayofaa ni ya kunyanyua Kwenye maeneo. yenye udongo wa kichanga au wakati wa kiangazi matuta ya makingo au meza. yanapendekezwa,Kutayarisha matuta, Debe Mbolea samadi au mboji Makapi ya Mpunga au mchanga Jembe Koleo Maji na Reki. Udongo kwenye kitalu unatakiwa uwe unaweza kupitisha maji vizuri Tayarisha kitalu chako kwa. kukwatua angalau Sm 20 kwenda chini ondoa mabaki yoyote ya mimea na mizizi na vunja. mabonge yote ya udongo, Pima upana na urefu wa kitalu ambao utakuwezesha kufikia kila pembe ya kitalu kwa urahisi. bila kukanyaga ndani ya kitalu Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kuleta magonjwa kwenye. kitalu na itarahisisha kung oa magugu pamoja na kuhamisha miche kwenda shambani Vipimo. vya tuta vinavyoshauriwa ni Sm 80 100 upana na urefu wowote kulingana na mahitaji yako. Changanya samadi iliyooza vizuri au mboji iliyoiva vizuri kwa uwiano wa debe 1 2 kwa mita. mraba Ongeza gram 10 vizibo viwili vya chupa ya maji za NPK au DAP au mbolea yoyote ya. kupandia kwa kila mita mraba Changanya udongo na mbolea vizuri na sawazisha na reki. hadi udongo uwe vizuri,Kutibu udongo kwenye tuta, Kama eneo hili limekuwa likilimwa mboga mara kwa mara tandaza majani makavu unene wa. sentimita 1 na choma juu yake ili kuua vimelea vya magojwa Baada ya kuchoma acha tuta. lipoe kwa siku 2 3 kabla ya kusia mbegu,Kusia mbegu. Panda au sia mbegu bora ambazo zimekomaa na kukauka vizuri ambazo hazijashambuliwa na. magonjwa au wadudu na zenye uwezo wa kuota vizuri zikipandwa Kama unahitaji kununua. mbegu inashauriwa kununua mbegu kutoka kwa mawakala wanaoaminika Siku moja kabla ya. kusia mbegu mwagia kitalu maji hadi kilowe vizuri, Mbegu zisiwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu.
kwenye tuta Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa. kwenye tuta kama mbegu ni ndogondogo sana Kama unasia mbegu katika mistari hakikisha. Kilimo bora cha mbogamboga, kuwa mistari ipo katika umbali wa sm 10 15 na kina cha sm 1 2 Baada ya kusia mbegu funikia. na udongo kidogo kutegemea na ukubwa wa mbegu, Mbegu zinaweza pia kusiwa kwenye tuta bila mistari lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri. kwenye tuta ili kupunguza msongamano Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama. vile kinyausi au kiuno damping off au ukungu blight. Matunzo ya kitalu, Baada ya kusia mbegu hakikisha kitalu hakipati jua la moja kwa moja na mvua kubwa Weka. matandazo ya majani ili kusaidia udongo kuhifadhi unyevunyevu na kuweza kuzuia mwangaza. wa jua wa moja kwa moja, Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye. udongo Mwagilia maji kidogo kidogo kwa utaratibu maalum hadi pale zitakapochipua mfano. kama unamwagilia asubuhi saa 4au 5 hakikisha kila siku unamwagilia mida hiyo hiyo ili kuzuia. uwezekano wa kutengeneza magojwa ya kwenye kitalu kama magonjwa ya ukungu Hakikisha. maji hayazidi kwenye kitalu kwani yanaweza kusababisha ugonjwa na miche kuharibika. Miche yote ikisha ota ondoa matandazo kisha weka kichanja ili kupunguza mionzi ya jua. ambayo inaweza kuunguza miche michanga kipindi cha baridi si muhimu sana Endelea. kumwagilia kwa utaratibu huo hapo juu, Hakikisha kitalu ni kisafi wakati wote Ondoa magugu yoyote yatakayojitokeza.
Punguzia miche kama imejazana sana ili kuipa nafasi ya kukua vizuri. Kagua kitalu mara kwa mara kuangalia kama kuna uvamizi wowote wa wadudu. waharibifu au mlipuko wa ugonjwa,2 BAADHI YA WADUDU NA MAGONJWA KWENYE KITALU. Sota Cut worm, Hawa ni wadudu mfano wa funza wakubwa wenye rangi ya kijivu ambao hukata miche karibu. na usawa wa ardhi Hujificha ardhini mchana na kutoka usiku kukata miche iliyoko kitaluni au. iliyopandwa muda huo huo Weka dawa kwenye udongo au ndani ya shimo kabla ya. kupandikiza miche, Nyunyiza dawa za kuua wadudu au majivu ya jikoni kwenye udongo au ndani ya shimo. kabla ya kupanda miche,Hakikisha miche inapata maji ya kutosha. Kilimo bora cha mbogamboga, Chimba kwenye shina lililokatwa na ukimpata mdudu huyu muue kwa mkono.
Ugonjwa wa Kiuno Damping off, Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia miche michanga kwenye shina usawa. wa ardhi Shina lililoshambuliwa hukauka na hatimaye mmea wote hunyauka na kukauka. Punguza miche ili kuruhusu hewa ya kutosha,Epuka kumwagilia juu ya mimea. Epuka sehemu inayotuamisha maji au kumwagilia maji mengi sana kwenye kitalu. Tumia dawa za ukungu kama vile Dithane M 45 Ridomil. Wadudu mafuta Aphids, Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi ya kijani nyeusi au kahawia Hukaa chini ya majani na. kufyonza utomvu kwenye majani machanga Mmea ulioshambuliwa hudhoofu hudumaa na. hatimaye hufa, Nyunyiza dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor Actellic Selecron Dursbanmaji. ya majani ya mwarobaini maji ya pilipili,Utiriri wa Mimea Red Spider Mites.
Ni wadudu wadogo sana ambao wana rangi ya machungwa yaliyoiva nyekundu au kahawia. Huonekana upande wa chini wa majani na hushambulia kwa kufyonza utomvu wake Majani. yaliyoshambuliwa huwa njano husinyaa hujikunja na hatimaye hukauka Majani. yaliyoshambuliwa pia huonyesha utando kama wa buibui. Weka maji ya kutosha kwenye mimea wakati wa kiangazi. Utitiri unazuiwa kwa kutumia dawa kama Abamectin, Magonjwa ya virusi Haya huenezwa na wadudu kama vile inzi weupe ambao mara nyingi. hushambulia mimea kwa kufyonza utomvu wake, Dalili za magonjwa ya virusi ni kujikunja kwa majani. Kilimo bora cha mbogamboga, Angamiza wadudu waenezao ugonjwa huu kwa kutumia madawa kama mwarobaini. Ng oa na kuchoma au kuchimbia ardhini mimea yote iliyona dalili za ugonjwa. 3 KUHAMISHA MICHE YA MBOGA MBOGA SHAMBANI, Mambo ya kuzingatia kabla ya kuhamisha miche ya mboga mboga shambani. Komaza miche kabla ya kuhamisha shambani kuizoesha mazingira magumu ili iweze. kukabiliana na mazingira halisi ya shambani Zoezi hili hufanyika kwa kuiacha miche ipate. mwanga wa jua kupunguza kivuli na kupunguza kumwagilia. Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamisha ili mizizi ishikamane vizuri na udongo. Mashimo yaandaliwe mapema katika nafasi zinazopendekezwa kwa zao husika Chagua miche. yenye afya nzuri mizizi mizuri na yenye majani kati ya 3 6 Miche ioteshwe siku hiyo hiyo ya. kungo a kutoka kitaluni Hamisha miche shambani wakati wa jioni kuepuka jua kali la mchana. Ngo a miche kwa uangalifu kupunguza uezekano wa kuharibu mizizi Mwagilia maji ya kutosha. mara baada ya kuotesha,MAANDALIZI YA SHAMBA LA NYANYA CHUNGU NGOGWE.
Shamba liandaliwe mapema angalau mwezi mmoja kabla ya kupanda na kuhamisha miche. shambani Tuta litibiwe kwa kuchoma nyasi juu ya udongo ili kuua vimelea vya magonjwa na. wadudu waharibifu wa mazao Miche huwa tayari kuhamisha baada ya wiki 5 ikiwa na urefu wa. sentimita 15 Kabla ya kung oa miche tuta linyeshwe ili kupunguza uwezekano wa kuua mizizi. Andaa tuta la upana wa mita moja na urefu wa kuanzia mita tano Chimba mashimo katika. nafasi na kisha weka mbolea ya samadi au mboji iliyoiva kiasi cha kutosha kutegemea na. rutuba ya eneo kati ya kilo moja hadi kilo mbili kwa shimo au debe moja katika kila mita moja ya. mraba Umbali wa upandaji hutegemea aina ya ngogwe ila kwa kawaida miche hupandwa. katika umbali wa sentimita 50 x 40 au 75 x 60,Kumwagilia. Hali ya unyevu katika ardhi ni muhimu hasa mimea inapokuwa katika hatua ya maua Hivyo ni. vyema ardhi iwe na unyevu wa kutosha wakati wote kwani ukame unaweza kusababisha. Kilimo bora cha mbogamboga, kuanguka kwa maua Inashauriwa kuweka matandazo wakati wa kiangazi ili kuhifadhi unyevu. Majani yasiwe karibu na shina kwa sababu inaweza kusababisha ugonjwa wa shina. NB Uoteshaji wa nyanya ni sawa na ngongwe,MAANDALIZI YA SHAMBA LA MNAVU. Shamba liandaliwe mwezi mmoja kabla ya kupanda kuhamisha miche Choma nyasi juu ya. udongo ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao Miche inakuwa tayari. kuhamisha kati ya wiki 4 6 ama miche ikiwa na majani 4 6. Andaa mashimo ya miche ya mnavu kulingana na idadi ya miche Weka mbolea Samadi mboji. ya kutosha kwenye mashimo Panda miche katika nafasi ya sentimita 30 50 na mstari hadi. mstari ni sentimita 50 Mwagilia baada ya kupanda kama udongo hauna unyevu Mwagilia maji. ya kutosha kwenye udongo siku 1 2 kabla ya kuhamisha miche shambani ili kupooza ardhi. Mambo ya kuzingatia baada ya kuhamisha miche ya mnavu. Mwagilia maji ya kutosha mara kwa mara kulingana na unyevu uliopo shambani. kisha weka matandazo kuhifadhi unyevu, Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo yaliyoko shambani. Shamba liwe safi wakati wote Ondoa magugu kwani yanaweza kuwa chanzo. cha wadudu na magonjwa, Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani.
Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema. Hakikisha shamba ni safi wakati wote palilia shamba na hakikisha magugu yote yamelimiwa. Umwagiliaji wa mimea ufanyike kwa mpangilio wa kudumu na maji safi yawekwe ya kutosha. kulingana na hali ya hewa, Weka uzio kuzunguka shamba au bustani ili kukinga mimea na upepo ambao unaweza kubeba. vimelea vya magojwa na wadudu kutoka sehemu moja hadi nyingine na kudhuru mimea yako. Kilimo bora cha mbogamboga, Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa kisha. zifukiwe chini au kuunguza moto, Kwa mimea ambayo mbegu zimeoteshwa moja kwa moja shambani punguza miche iliyoota. zaidi ya idadi inayotakiwa kwenye shimo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye mimea. pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya. wadudu maadui kwenye mimea hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea. unyevunyevu, Mbinu za msingi za kuthibiti magonjwa na wadudu katika kilimo cha mboga. Madhara ya magonjwa na wadudu, a Hupunguza kiasi cha mavuno na hata kuua mimea kabisa.
b Hupunguza ubora wa mboga, c Huongeza gharama za uzalishaji hasa madawa ya viwandani yanapotumiwa. d Huongeza uharibifu wa mboga baada ya kuvuna, Namna ya kutambua magonjwa na wadudu washambuliao mboga. Kila aina ya mboga ina namna yake ya utunzaji kwani zinashambuliwa na aina tofauti ya. magojwa na wadudu Hivyo ni lazima utambue aina ya ugonjwa au mdudu ili utumie kinga. inayostahili Hii siyo kazi rahisi, Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kutumika. Kutumia uzoefu wako hasa baada ya kuwa na wataalam wa wadudu na magonjwa ya. mimiea kwa muda mrefu,Kutumia mabwana shamba, Peleka kuchunguza sehemu ya mmea uliyougua kwenye maabara za mimea. Kanuni za kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu. Kabla hujaamua kutumia madawa ya kienyeji au viwandani hakikisha unafanya mambo. yafuatayo katika bustani yako, Chagua udongo usiokuwa na magonjwa ya mboga unayotaka kuzalisha.
Kilimo bora cha mbogamboga, Rutubisha udongo na mimea kwa kutumia mbolea za asili na za viwandani kama zinapatikana. Tumia mbegu bora kwani baadhi ya magonjwa hutokana na mbegu Pia chagua aina za mbegu. bora ambazo huvumilia magojwa na wadudu, Hakiksha kuwa vitalu bustani na sehemu ya kuhifadhi mboga ni safi Uchafu na magugu. huvutia magonjwa na wadudu waharibifu, Toa majani au mimea iliyokwisha ugua na ichome moto au ifukie. Panda mazao muda unaotakiwa ili kukwepa baadhi ya magonjwa ya msimu. Epuka kupanda mboga ya jamii moja katika eneo moja kwa misimu mingi mfululizo. Changanya mazao au mimea ambayo inafukuza magonjwa na wadudu kama vile mimea. Epuka kuchanganya mboga na baadhi ya mazao yanayovutia magonjwa au wadudu katika. bustani yako Mfano mazao kama mipapai na bamia huvutia nzi wadogo weupe wanaoeneza. ugonjwa wa ukoma wa nyanya, Mwisho tumia madawa ya asili na viwandani ili kupunguza kuenea kwa magonjwa na wadudu. Kubadilisha mazao shambani, Kubadilisha mazao shambani ni utaratibu wa kuacha kupanda mfululizo aina ileile ya zao katika.
eneo hilo hilo Iwapo eneo ni kubwa bustani igawanywe katika sehemn tatu au nne ili kuepuka. kupanda mfululizo aina ileile ya zao Katika kila sehemu panda aina nyingine ya mazao na ya. familia tofauti kila baada ya kuvuna, Baada ya kuvuna mazao ya sehemu ya kwanza yapandwe katika sehemu ya pili ya pili katika. sehemu ya tatu na ya tatu yapandwe katika sehemu ya nne na yale ya nne yapandwe katika. sehemu ya kwanza, Kubadilisha mazao shambani huzuia ongezeko la wadudu na magonjwa yanayoshambulia jamii. moja ya zao Vilevile huhifadhi rutuba ya udongo na huzuia uotaji wa magugu Utaratibu huu pia. humwezesha mkulima kuweka kiasi cha mbolea kinachotakiwa shambani Ufuatao ni mfano wa. kubadilisha mazao,Kilimo bora cha mbogamboga,Mfano wa kubadilisha mazao. Jamii ya Nyanya Jamii ya Matango,Biringanya Matango. Nyanya Maboga,Pilipili Matikiti Maji,Viazi Mviringo.
Jamii ya Mizizi Jamii ya kabichi,Karoti Kabichi,Vitunguu Sukuma wiki. Kanuni za kukinga magonjwa na wadudu kwa kutumia madawa. Unalazimika kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu kwa kutumia madawa ya asili na. viwandani pale mbinu nyingine ambazo zimetajwa hapo nyuma zinaposhindwa kuleta. Zifuatazo ni baadhi tu ya kanuni za kutumia madawa ya asili na viwandani. Kwa usalama wa mlaji unashauriwa kupiga madawa hasa ya viwandani siku 14 kabla ya. kuvuna mboga hapa zingatia shelf life ya dawa kama ilivyo kwenye lebo Pia epuka kupiga. madawa mara kwa mara, Epuka kupiga dawa ya aina moja mara kwa mara dhidi ya ugonjwa au mdudu wa aina moja. kwani kufanya hivyo huwafanya wadudu kujenga sugu dhidi ya dawa hiyo. Epuka kupiga dawa wakati wa upepo mkali au jua kali sana kwani kiasi kikubwa cha dawa. kinaweza kupotea hewani Pia usipige dawa wakati wa mvua mara tu kabla ya mvua kwani. maji ya mvua yataosha na kupunguza nguvu ya dawa,Kilimo bora cha mbogamboga. Piga dawa ya kutosha sehemu zote za mmea kwani baadhi ya wadudu au magonjwa hukaa na. kushambulia sehemu ya chini ya majani, Andaa vizuri bomba la kupigia dawa kabla ya kuchanaganya dawa na maji ili dawa iweze. kutoka vizuri, Madawa hutofautiana sana nguvu za kuua wadudu hivyo changua madawa yanayofaa.
kufuatana na ugonjwa na wadudu, Piga dawa wakati wa asubuhi hasa kukinga magonjwa ya ukungu yapendayo unyevunyevu. Kwa kuzuia wadudu ni vizuri kupiga dawa wakati wa jioni Wakati wa jioni dawa huua wadudu. zaidi kwani hukaa muda mrefu juu ya majani kabla ya nguvu yake kuharibiwa na jua. Weka kiwango cha dawa kama ilivyo elekezwa na watengenezaji au watalaam Kiasi kidogo. cha dawa katika maji hufanya viini vya magonjwa na wadudu kuwa sugu. Zingatia kuwa kiasi cha sumu ndani ya kasha au kopo la dawa hutofautiana kati ya kampuni na. kampuni iliyotengeneza, Ikiwezekana tafuta ushauri kwa muuza madawa au wataalam waliokaribu nawe. Baadhi ya madawa ya asili, Madawa ya asili ni mengi ila bado hajafanyiwa utafiti wa kutosha. Baadhi ya mimiea inayotoa madawa ya asili ambayo yameshajaribiwa Tanzania ni muarobaini. mbegu na majani kitunguu swaumu manung anung a tumbaku pilipili kali pareto n k. Muarobaini ni miongoni mwa mimea michahce ambayo mpaka sasa imefanyiwa utafiti wa kina. Mfano kuchanganya nusu kilo ya mbegu za muarobaini zilizotwangwa katika lita ishirini za maji. husaidia kuua wadudu mbalimbali wakiwemo funza wanaotoboa matunda ya mboga mboga. kama nyanya, Kuchanganya kilo moja ya majani ya mwarobaini yaliyotwangwa kwenye lita 10 za maji pia. huua wadudu mbalimbali wa mbogamboga,Uzuri na kasoro ya madawa ya asili.
Kilimo bora cha mbogamboga, Madawa ya asili ni bora zaidi kuliko madawa ya viwandani kwani sumu yake ni kidogo na. hupungua nguvu haraka baada ya kupiga dawa, Hivyo ni salama zaidi kwa mpigaji dawa na mlaji mboga Hivyo kupendekezwa katika kilimo hai. na hifadhi ya mazingira, Kasoro kubwa katika kutumia madawa ya asili ni kama zifuatayo. Hayajafanyiwa utafiti wa kutosha ukilinganisha na yale ya viwandani Mfano dawa ipi inayofaa. kwa mdudu yupi, Yanakinga zaidi mboga dhidi ya wadudu waharibifu kuliko magonjwa. Uwiano wa kuchanganya dawa na maji bado haujulikani vizuri Mfano kiwekwe kiasi gani cha. dawa katika kiasi gani cha maji, Kwa kuwa nguvu yake ni kidogo hayatafaa kuzuia mashambulizi makubwa ya magonjwa au.
Uzuri na kasoro za madawa ya viwandani, Madawa ya viwandani yana sumu nyingi zaidi na hivyo huzuia haraka zaidi mashambulio ya. magonjwa na wadudu Hivyo hutumika sana katika kilimo cha mboga na mazao mbali mbali. kuliko madawa ya kienyeji Tatizo la haya madawa ni kwamba ni hatari kwa mkulima mlaji wa. mboga mazingira na pia gharama zake ni kubwa,Matumizi ya madawa. Ni muhimu kutumia madawa ili kukinga mimea kutokana na athari za wadudu na magonjwa. Hata hivyo madawa yatumike pale inapobidi kwani ni ghali na yana madhara kwa mazingira na. Kilimo bora cha mbogamboga, Mambo yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kutumia madawa Hakikisha unatumia. dawa inayoshauriwa na wataalamu, Soma kwa uangalifu maelezo yanayoambatana na dawa toka kwa watengenezaji kabla. ya kutumia na yasikiukwe Hii itakusaidia kujua vifaa kiasi na jinsi ya kutumia Madawa. ni hatari kwa binadamu na wanyama kama yatatumika isivyopasa. Wakati wa kuchanganya na kunyunyizia dawa vaa nguo na vifaa vya kinga Vifaa hivi ni. kofia glovus viatu gumboots kitambaa cha kufunika mdomo na pua miwani na. Tumia maji safi kuchanganya dawa, Epuka kuvuta hewa yenye dawa Wakati wa kunyunyizia dawa usielekee upepo.
unakotoka bali elekea upepo unakoenda, Usile wala kuvuta wakati wa kuchanganya au kunyunyizia dawa. Baada ya kunyunyizia dawa osha mwili kwa sabuni na maji mengi na safi. Maji yanayotumika kusafishia bomba yasimwagwe katika maji yaliyotuama au. yanayotembea kwani yanaweza kuleta madhara sehemu nyingine Maji yamwagwe. kwenye shimo na kufukiwa, Nguo na vifaa vingine vilivyotumika zifuliwe mara moja kwa sabuni na maji safi. Osha vizuri mikono kwa sabuni kabla ya kula kunywa chochote au kuvuta sigara. Makopo au chupa zilizokuwa na dawa zisitumike bali ziharibiwe na kufukiwa. Hifadhi madawa mahali salama na pasipofikiwa na watoto kwa urahisi Dawa ziachwe. katika makasha chupa au makopo yake zilimokuwemo Hata siku moja madawa ya. mimea yasitumike kwa kutibu binadamu, Endapo kutakuwepo na matatizo yeyote katika matumizi muone Mtaalamu kwa ushauri. Iwapo sehemu ya kutolea dawa itaziba tumia nyasi au kijiti kuzibua Kamwe usizibue.

Related Books

Revised Pages Key to the Genera of Leptosporangiate and ...

Revised Pages Key to the Genera of Leptosporangiate and

Revised Pages Ferns 65 Key to the Genera of Leptosporangiate and Eusporangiate Ferns (Polypodiopsida) as Found in Michigan 1. Plants aquatic or partially so; small and free-floating or clover-shaped and

ANALYSIS OF INTERNAL BONDED FIBRE REINFORCED COMPOSITE ...

ANALYSIS OF INTERNAL BONDED FIBRE REINFORCED COMPOSITE

used to rehabilitate internally corroded pipeline to prevent further corrosion. The high tensile strength, lightweight, durability and versatility of fibre composites makes them the material of choice for many repair and rehabilitation projects (Elsani 2009). These properties combined with the direction dependency allow the

Denso Protal 7200 is used in the rehabilitation of a ...

Denso Protal 7200 is used in the rehabilitation of a

Denso Protal 7200 is used in the rehabilitation of a pipeline in the USA - see story page 4-5. 2 WINN & COALES INTERNATIONAL LTD WINN & COALES (DENSO) LTD Tel: +44 (0) 20 8670 7511 Denso House, Chapel Road, London SE27 OTR, England Fax: +44 (0) 20 8761 2456 Anti-corrosion and sealing systems Email: mail@denso.net Website: www.denso.net ARCHCO-RIGIDON Tel: +44 (0) 20 8761 6244 Denso House .

Autodesk TinkerCoding Badge Guide - Amazon S3

Autodesk TinkerCoding Badge Guide Amazon S3

Autodesk TinkerCoding Badge Guide (Version 2/23/15) Abstract: Building a Configurable House with Tinkercad ... personalize your Tinkercad house shape or create an entirely new shape/design from scratch on your own. To claim your virtual badge, upload your creation from Activity 3. After you claim your virtual TinkerCoding badge, please see your dojo leader for your TinkerCoding laptop badge ...

Best Practices for High Density Wireless Network Design In ...

Best Practices for High Density Wireless Network Design In

The following design recommendations are best practices based on many successful installations and should serve as guidelines for proper design, planning, and deployment of a wireless network in a high density environment. 1) Identify High Density Areas - start the design process by using a live RF tool such as AirMagnet planner to identify

N1470(E)(M30)H JUNE EXAMINATION NATIONAL CERTIFICATE

N1470 E M30 H JUNE EXAMINATION NATIONAL CERTIFICATE

1.4 Explain how the consultants at Travel Options can use the following forms of non-verbal communication effectively. 1.4.1 Music 1.4.2 Kinesics 1.4.3 Colour (3 x 2) (6) 1.5 The space around people can be divided in four different zones. Name the FOUR zones and briefly describe each. (4 x 2) (8) 1.6

COMMERCE - Past Papers Of Home

COMMERCE Past Papers Of Home

The multiple choice paper consists of 40 4-option items with some questions involving pictorial or diagrammatic data such as Questions 1 , 14 , 19 , 23 , 24 and 37 and some requiring candidates to undertake

Supplier Responsibility - Apple Inc.

Supplier Responsibility Apple Inc

conduct onsite meetings to review gap analysis of low-score areas, identify the root cause of all issues, and develop with our supplier partners a customized corrective action plan. During this process, we draw upon a bank of over 100 technical toolkits assembled from our extensive experience in building supplier capability. Over a period of three to six months following an assessment, Apple ...

Processing speech signals for disabilities

Processing speech signals for disabilities

tactile, or direct electrical stimulation ofthe auditory nerve (auditory-neural)] but also in terms ofthe degree ofspeech processing that is used. At least four such categories canbe distinguished: assistive devices (a) that are not designed specifically for speech, (b) that take the average characteris-tics of speech into account, (c) that process articulatory or phoneticcharacteristics ...

RFID Essentials - Ommolketab.ir

RFID Essentials Ommolketab ir

RFID technologies laid out in RFID Essentials with modern business integration using service-oriented architectures. This is the book to read in order to understand this new landscape."--Mark Bauhaus, Senior Vice President, Sun Microsystems, Inc. "This is a must read for RFID Software and Solution architects and is highly recommended for anyone needing to gain more insight into the myriad of ...