Usawiri Wa Mhusika Padri Katika Riwaya Za Kezilahabi-Books Pdf

USAWIRI WA MHUSIKA PADRI KATIKA RIWAYA ZA KEZILAHABI
14 Jan 2020 | 333 views | 2 downloads | 94 Pages | 555.10 KB

Share Pdf : Usawiri Wa Mhusika Padri Katika Riwaya Za Kezilahabi

Download and Preview : Usawiri Wa Mhusika Padri Katika Riwaya Za Kezilahabi

Report CopyRight/DMCA Form For : Usawiri Wa Mhusika Padri Katika Riwaya Za KezilahabiTranscription

USAWIRI WA MHUSIKA PADRI KATIKA RIWAYA ZA, KEZILAHABI. Uchunguzi katika Rosa Mistika Gamba la Nyoka na Nagona. Peres Gregory Mosha, Tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kukamilisha masharti ya Digirii ya M A. Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Oktoba 2013, UTHIBITISHO, Aliyetia saini hapa chini anathibitisha kwamba amesoma tasinifu hii USAWIRI. WA MHUSIKA PADRI KATIKA RIWAYA ZA KEZILAHABI Uchunguzi. katika Rosa Mistika Gamba la Nyoka na Nagona na kupendekeza ikubaliwe na. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa minajili ya kukamilisha masharti ya Digirii ya. M A Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt A K Mutembei.
HAKIMILIKI, Mimi Peres Gregory Mosha nathibitisha kwamba tasinifu hii ni kazi yangu. mwenyewe na haijawahi kuwasilishwa na haitawasilishwa katika Chuo Kikuu. kingine chochote kwa ajili ya kutunukiwa Digrii kama hii au Digrii nyingine yoyote. Haki ya kunakili tasinifu hii inalindwa na Mkataba wa Berne Sheria ya Haki ya. Kunakili ya mwaka 1999 na Mikataba mingine ya kitaifa na kimataifa inayolinda. mali za kitaaluma Haki zote zimehifadhiwa Hairuhusiwi kuiga kunakili au. kutafsiri kwa njia yoyote ile au kwa mfumo wowote ule ama iwe ni yote au sehemu. ya tasinifu hii bila ya idhini ya maandishi kutoka ofisi ya Kurugenzi ya Masomo ya. Uzamili kwa niaba ya mwandishi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kinachoruhusiwa ni madondoo mafupi mafupi kwa makubaliano halali kwa ajili ya. tafiti tahakiki au mijadala ya kitaaluma, Kwa hakika si kazi rahisi kuwataja na kuwashukuru kwa majina wote waliochangia. kukamilika kwa utafiti huu Napenda kutumia fursa hii kutoa shukrani zangu za. dhati kwa wote ambao wamewezesha kukamilika kwa utafiti huu Wafuatao. wanastahili shukrani za pekee, Kwanza namshukuru msimamizi wangu Dkt A K Mutembei kwa kukubali. kunisimamia na kuhakikisha kuwa ninaukamilisha utafiti huu Kwa hakika mawazo. yake na ushauri wake vimekuwa na msaada mkubwa sana kwangu katika. kuukamilisha utafiti huu, Pili Naushukuru uongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mwenge na kwa. kipekee Mkuu wa Chuo Dkt Filbert Vumilia kwa kukubali kufadhili masomo yangu. katika kiwango cha shahada ya umahiri katika Kiswahili. Tatu ninapenda kuwashukuru wahadhiri wote katika Taasisi ya Taaluma za. Kiswahili TATAKI walionifundisha na kutoa muda wao wa thamani kunishauri na. kunielekeza Kipekee namshukuru Prof M M Mulokozi kwa kupitia wazo la utafiti. na kulifanyia marekebisho pamoja na kutoa maoni yake pale alipoona yafaa Hakika. mawazo yake yalinipa ari ya kuendelea na utafiti huu katika ngazi ya pili ya. pendekezo la utafiti, Mwisho lakini si kwa umuhimu nawashukuru wanafunzi wenzangu wote wa Digrii.
ya M A Kiswahili kwa mwaka wa masomo 2011 2012 Kipekee niwashukuru Aneth. Kasebele Jubeck Masebo Nsia Kweka Martha Mageni na Scolastica M John. Naitabaruku tasinifu hii kwanza kwa watoto yatima wote duniani Mungu ni baba. yenu Pili kwa wote wanaopitia hali ngumu Kumbukeni kuwa mkiisha kupitia. hali ngumu mtakuwa wagumu na hatimaye hali ngumu zitawaogopa kwa sababu ya. ugumu wenu na zitawakimbia Tatu kwa watoto wangu wapenzi Holiness Peres na. Faith Peres kwa uvumilivu wao kwa kipindi chote nilichokuwa masomoni Ninyi ni. nguvu zangu, Utafiti huu unahusu usawiri wa mhusika Padri katika riwaya za Kezilahabi. uchunguzi unaofanyika katika Rosa Mistika 1971 Gamba la Nyoka 1979 na. Nagona 1990 Utafiti huu ulijikita katika malengo makuu matatu Mosi. kuchambua uhusika wa mhusika Padri katika riwaya teule pili kujadili dhamira. zinazowasilishwa na mhusika Padri katika riwaya teule na tatu kubainisha motifu. inayojitokeza kupitia mhusika Padri katika riwaya teule Mtafiti alifuatilia hatua kwa. hatua matendo ya mhusika Padri maneno yake na yale ambayo wahusika wengine. wanasema kumhusu Kupitia mambo haya ilibainika kuwa mhusika Padri. anasawiriwa katika nafasi mbalimbali kama vile Padri kama kiongozi wa Kanisa. katika jamii ambapo ana jukumu la malezi ya kiroho na kufanya shughuli za ibada. Padri kama mwanamume wa kawaida katika jamii ambapo anaonekana katika. matendo kama vile uzinzi ulevi ugomvi na kadhalika Pia tumeona kuwa mhusika. Padri anatokea kama mtu mwenye sauti katika jamii na kama mwelekezaji Utafiti. huu pia ulibaini kuwa mhusika Padri katika riwaya teule za Kezilahabi anawasilisha. dhamira kuu nne ambazo ni suala la malezi ya kiroho unafiki wa viongozi wa. Kanisa Katoliki Uonevu na kukosekana haki na suala la uwezo wa Padri kuondoa. dhambi Kwa kutumia nadharia ya uhalisia wa Kimarx tuliona kwa mifano. mbalimbali kwamba matendo yanayojadiliwa katika riwaya za Kezilahabi kupitia. mhusika Padri ni halisi katika jamii Aidha tumebaini kwamba motifu ya Padri. aliyeshindwa inajitokeza katika riwaya teule za Kezilahabi Hii ni aina mpya ya. motifu katika fasihi ya Kiswahili Tumebaini pia kuwa mhusika Padri si mhusika wa. kawaida bali ni mhusika wa kimotifu mhusika anayewakilisha motifu. Uthibitisho ii, Ikirari na Hakimiliki iii, Shukrani iv. Tabaruku v, Ikisiri vi, SURA YA KWANZA UTANGULIZI WA UTAFITI 1. 1 1 Utangulizi 1, 1 2 Usuli 1, 1 3 Tatizo la Utafiti 3. 1 4 Malengo ya Utafiti 5, 1 5 Maswali ya Utafiti 6.
1 6 Umuhimu wa Utafiti 6, 1 7 Mawanda ya Utafiti 7. 1 8 Hitimisho 7, SURA YA PILI MAPITIO YA MAANDIKO NA KIUNZI CHA NADHARIA 9. 2 1 Utangulizi 9, 2 2 Tafiti Tangulizi na Mapitio ya Maandiko 9. 2 3 Kiunzi cha Nadharia 16, 2 4 Hitimisho 18, SURA YA TATU MBINU ZA UTAFITI 19. 3 1 Utangulizi 19, 3 2 Mbinu za Ukusanyaji Data 19.
3 3 Sampuli na Usampulishaji 21, 3 4 Uchambuzi Uchakataji na Uwasilishaji wa Data 22. 3 5 Vifaa vya Utafiti 23, 3 6 Eneo la Utafiti 23, 3 7 Hitimisho 24. SURA YA NNE UCHAMBUZI WA DATA MATOKEO YA UTAFITI NA. MJADALA 25, 4 1 Utangulizi 25, 4 2 Rosa Mistika 25. 4 2 1 Utangulizi 25, 4 2 2 Uhusika wa Mhusika Padri katika Rosa Mistika 26. 4 2 3 Mhusika Padri kama Mtumishi wa Kanisa katika Jamii 27. 4 2 3 1 Mhusika Padri kama Mlezi wa Kiroho 27, 4 2 3 2 Mhusika Padri kama Kiongozi wa Ibada 31.
4 3 Gamba la Nyoka 32, 4 3 1 Utangulizi 32, 4 3 2 Mhusika Padri katika Gamba la Nyoka 32. 4 3 2 1 Padri kama Kiongozi wa Kanisa katika Jamii 33. 4 3 2 2 Padri kama Mwanaume wa Kawaida katika Jamii 34. 4 4 Nagona 40, 4 4 1 Utangulizi 40, 4 4 2 Padri kama Mtu Mwenye Sauti katika Jamii 41. 4 4 3 Padri kama Mtu Mwenye Uwezo Kuliko Wengine 41. 4 4 4 Padri kama Mwelekezaji Mwonyesha Njia 42, 4 4 5 Padri kama Mlevi katika Jamii 43. 4 4 6 Padri kama Mtu asiye na Heshima kwa Wazee 44. 4 4 7 Padri kama Binadamu wa Kawaida 44, 4 5 Dhamira Zinazowasilishwa na Mhusika Padri 45. 4 5 1 Utangulizi 45, 4 5 2 Suala la Malezi ya Kiroho 45.
4 5 3 Unafiki wa Viongozi wa Kanisa Katoliki 47, 4 5 4 Uonevu na Kukosekana kwa Haki 49. 4 5 5 Suala la Uwezo wa Padri kuondoa Dhambi 50, 4 6 Motifu Inayojitokeza kupitia Mhusika Padri 52. 4 6 1 Utangulizi 52, 4 6 2 Motifu ya Padri Aliyeshindwa 53. 4 6 3 Mhusika wa Kimotifu Mhusika anayewakilisha motifu 56. 4 7 Mjadala wa Matokeo ya Utafiti 57, 4 7 1 Mhusika Padri Anavyoelezewa katika Riwaya za Kezilahabi 57. 4 7 2 Tofauti za Uwasilishaji wa Mhusika Padri katika Riwaya za Kezilahabi 61. 4 7 3 Dhamira Zinazowasilishwa na Mhusika Padri 62. 4 7 3 1 Dhamira ya Malezi ya Kiroho 62, 4 7 3 2 Dhamira ya Unafiki wa Viongozi wa Kanisa Katoliki 63.
4 7 3 3 Dhamira ya Uonevu na Kukosekana kwa Haki 67. 4 7 3 4 Dhamira ya Uwezo wa Padri Kuondoa Dhambi 67. 4 7 4 Motifu ya Padri Aliyeshindwa 68, 4 8 Ufaafu wa Nadharia ya Uhalisia wa Kimarx Tuliyoitumia 69. 4 9 Hitimisho 70, SURA YA TANO MUHTASARI HITIMISHO NA MAPENDEKEZO 72. 5 1 Utangulizi 72, 5 2 Muhtasari Kuhusu Utafiti 72. 5 3 Matokeo ya Utafiti na Ugunduzi 73, 5 4 Mchango wa Utafiti 75. 5 5 Mapendekezo kwa Tafiti Zijazo 76, MAREJELEO 77.
VIAMBATANISHO 80, SURA YA KWANZA, UTANGULIZI WA UTAFITI. 1 1 Utangulizi, Utafiti huu unahusu usawiri wa mhusika Padri katika riwaya za Kezilahabi za Rosa. Mistika 1971 Gamba la Nyoka 1979 na Nagona 1990 Katika kazi zake. mbalimbali Kezilahabi amemtumia mara nyingi Padri kama mhusika kuliko. alivyowatumia wahusika wengine Jambo hili limevuta hamu ya utafiti kutaka kujua. ni kwa nini hasa mhusika huyu amemvutia mwandishi na hasa kutaka kumjua kwa. undani mhusika mwenyewe Katika kufanya utafiti huu lengo ni kujadili dhamira. zinazowasilishwa na mhusika Padri katika riwaya hizo na kubainisha motifu. inayojitokeza kupitia mhusika Padri katika riwaya teule. Sura hii imegawanywa katika sehemu saba sehemu ya kwanza inaeleza utangulizi. wa sura hii sehemu ya pili usuli wa tatizo la utafiti sehemu ya tatu inaeleza tatizo la. utafiti sehemu ya nne inaeleza malengo ya utafiti sehemu ya tano inaeleza juu ya. maswali ya utafiti sehemu ya sita inaeleza umuhimu wa utafiti na sehemu ya saba. inaeleza mawanda ya utafiti na sehemu ya nane ni hitimisho la sura hii. Wataalamu mbalimbali Mlacha 1985 1986 1987 Madumulla 1987 2009. Wamitila 2002 Ntarangwi 2004 Njogu na Chimerah 2008 Senkoro 1982 2011. wameshughulikia wahusika katika fasihi ya Kiswahili na wote kwa namna moja au. nyingine wanakubaliana kuwa wahusika ni viumbe waliokusudiwa kuwakilisha. tabia za watu katika kazi ya fasihi, Mathalan Mlacha 1985 30 anasema riwaya yoyote haikosi mhusika na mara. nyingi huwapo wahusika kadhaa Anaendelea kusema kuwa wahusika ni watu. ambao msanii mwenyewe huwabuni kutokana na maisha ya jamii yake kulingana na. kile anachotaka kukifafanua Akifafanua umuhimu wa uhusika katika nathari. Mlacha 1986 anasema uhusika ni moja kati ya vipengele muhimu sana vya. nathari Nafasi na dhima ya mhusika vina umuhimu mkubwa katika muundo wa. matini tafsiri ni yetu, Kutokana na mambo haya mawili jinsi wahusika wanavyobuniwa na dhima yao. katika kazi ya kifasihi tunaona kuwa uumbaji wa mhusika Padri katika kazi za. Kezilahabi haukutokea kibahati nasibu Mwandishi bila shaka alikuwa na lengo. fulani na amemtumia mhusika wake kurejelea lengo hilo. Msokile 1992 42 anasema wahusika katika kazi yoyote ya sanaa itumiayo lugha. ni watu wanyama ama vitu Wahusika hao husawiriwa kisanaa na mwandishi ili. waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii Kwa hiyo. mwandishi huwasawiri wahusika kwa wasomaji wake kwa kutumia sifa pambanuzi. walizo nazo namna gani walivyo mambo gani hawayapendi na yapi wanayapenda. na maisha yao Tunaamini kuwa mwandishi kwa kumtumia mhusika Padri zipo. dhana ambazo alikusudia kuziwasilisha kwa jamii kupitia sifa pambanuzi alizo nazo. mhusika huyo na namna alivyo, Mbali na wahusika kwa ujumla mhusika Padri ametumiwa na waandishi kadhaa.
Katika kazi mbalimbali za fasihi zikiwemo za riwaya ya Kiswahili mhusika Padri. amejitokeza kwa namna tofauti Mhusika huyu kwa mfano anatokea katika riwaya. ya Juan Rulfo Pedro P ramo 1955 riwaya ya Pete ya Komba 1986 riwaya ya. Janga Sugu la Wazawa ya Gabriel Ruhumbika 2001 na katika riwaya tatu za. Euphrase Kezilahabi yaani Rosa Mistika 1971 Gamba la Nyoka 1979 na. Nagona 1990 na kwa sehemu ndogo sana katika Mzingile 1991. Kwa kuwa mhusika Padri amejitokeza mara nyingi katika riwaya ya Kiswahili na. zaidi katika riwaya za Kezilahabi tumevutiwa kufanya utafiti kumhusu yeye. miongoni mwa wahusika wengine kutokana na namna alivyotumika Aidha kwa. kuwa mwandishi ni miongoni mwa magwiji wa fasihi ya Kiswahili bila shaka kwa. kumtumia Padri alikuwa na lengo mahususi Hivyo basi utafiti huu unakusudia. kuchunguza usawiri wa mhusika Padri katika riwaya tatu za Kezilahabi ambazo ni. Rosa Mistika 1971 Gamba la Nyoka 1979 na Nagona 1990. 1 3 Tatizo la Utafiti, Licha ya wanafasihi mbalimbali kama vile Senkoro 1976 Gibbe 1982 Senkoro. 1982 2011 Mulokozi 1983 Madumulla 1987 Mlacha 1986 1987 1988 1991. Wamitila 1991 1998 2003 Bertoncini 1992 Gromov 1998 Mbatiah 1998 Diegner. 2002 Mwangoka 2011 kwa kutaja tu baadhi kushughulikia riwaya za Kezilahabi. na kugusia wahusika kwa namna moja au nyingine bado kuna pengo la kiuchambuzi. kumhusu mhusika Padri Mtazamo wa wanafasihi na watafiti walio wengi umekuwa. ni kuwashugulikia wahusika kwa kuzingatia nafasi zao katika riwaya na si uhusika. wao Kwa hiyo uchambuzi na uhakiki haujawagusa wahusika kutokana na uhusika. wao kama viongozi wa siasa au dini au serikali n k Swali tunalojiuliza hapa ni je. ni nini maana ya uhusika wa kiongozi kama huyu katika nafasi yake ya kazi katika. jamii halisi yaani jamii nje ya riwaya Kwa mfano Kezilahabi anamtumia mhusika. Malyangu ambaye ni katibu Mkuu wizarani Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani. Je ni nini athari na maana pana ya dhima ya makatibu wakuu wa wizara kwa namna. wanavyotazamwa na mwandishi Vivyo hivyo kwa mhusika wa kisiasa au kidini. kama alivyotumika Padri, Uchambuzi wa mhusika Padri umefanywa kwa uchache na Wamitila katika makala. zake mbalimbali 1991 1998 na 2003 Kwa mfano katika makala yake. inayojulikana kama A Philosophical Labyrinth Tracing two Critical Motifs in. Kezilahabi s Prose Works Wamitila 1998 anaizungumzia riwaya ya Rosa Mistika. kwa kusema kuwa mwandishi anaonesha mapungufu ya Ukristo wakati Padri wa. Kikatoliki anapokwenda kumshauri Rosa lakini hachukui hatua yoyote ya. kuzungumzia matatizo yake Rosa ya hapa hapa duniani na badala yake anaegemea. zaidi kwenye maono ya kesho nzuri tafsiri ni yetu Akimwangalia Padri katika. Gamba la Nyoka Wamitila keshatajwa uk 84 anaendelea kudai kwamba matumizi. ya Padri yanaendeleza unafiki mkubwa na ulioenea katika Ukristo Kupitia kwa. Padri Madevu na mmoja wa wafuasi wake waaminifu Mama Tinda dhamira . Janga Sugu la Wazawa ya Gabriel Ruhumbika 2001 na katika riwaya tatu za Euphrase Kezilahabi yaani Rosa Mistika 1971 Gamba la Nyoka 1979 na Nagona 1990 na kwa sehemu ndogo sana katika Mzingile 1991 Kwa kuwa mhusika Padri amejitokeza mara nyingi katika riwaya ya Kiswahili na

Related Books

M THODE MINCEUR 7jours Teleshopping

M THODE MINCEUR 7jours Teleshopping

M thode Minceur 7 Jours Notre M thode Minceur 7 Jours est test e cliniquement et comporte 2 phases u Une phase d attaque la m thode en route pour la minceur en 7 jours seulement u Obligatoirement poursuivie de la phase stabilisation de 7 jours de la m thode je garde ma ligne Le Potage Di t tique La m thode comprend le potage et son livret de la m thode

plancha Francis Batt

plancha Francis Batt

secrets pour vous et donneront un air de voyage vos grillades Savourez des burgers pr par s avec des pains faits maison et ma trisez la plancha avec des cuissons simples et rapides R tissez des grosses pi ces de viande grillez tous les l gumes pour des saveurs incomparables utilisez la grillade pour donner du fondant au fromage

JUSQU AU 13 JANVIER 2018 70

JUSQU AU 13 JANVIER 2018 70

LE BLENDER Ultra puissant fourni avec deux jeux de lames Lame blender smoothie pour mixer et m langer fruits et l gumes Lame hachoir broyeur pileur glace pour broyer pices noix et grains de caf 220 240 V 1000 W Lame blender smoothie Lame hachoir broyeur pileur glace 4 mugs 0 25 L avec couvercle Petit 0 5 L et grand bol 1 L Couvercle emporter 2

About me About the book Blender

About me About the book Blender

secrets and cool tricks as I could stuff in along the way To explain why certain choices were made and what some other alternatives are Goals and Approach Much of the book centers around creating and animating a single character Captain Blender Can be followed in several ways Most intensive do all the tuts from the beginning Less intensive follow selected tuts

Qui tique encore sur l Ortie qui pique Free

Qui tique encore sur l Ortie qui pique Free

liquide passer le tout au blender pendant 1mn c est pr t Bi re d orties Recette de Bernard Bertrand dans Les secrets de l Ortie propos e par Christian Pour 5 l de boisson faire bouillir doucement dans de l eau durant 40mn 500g de jeunes orties avec 1 citron coup en tranches zeste compris Faites dissoudre 250 300g de sucre roux puis d layer dans un peu de liquide ti de

SVG to RDF Image Semantization CORE

SVG to RDF Image Semantization CORE

SVG to RDF Image Semantization Khouloud Salameh1 Joe Tekli2 based on a combination of shape color and position similarity measures Our method presents several advantages namely i achieving complete semantization of image content ii allowing semantic based data search and processing using standard RDF technologies iii while being compliant with Web standards i e SVG and RDF

Antimicrobial potential activity of leaf extracts of

Antimicrobial potential activity of leaf extracts of

also be checked when used in combination with other herbal drugs Catharanthus roseus L which is an important medicinal plant of the family Apocynaceae is used to treat many of the fatal diseases C roseus also possess good antioxidant potential There are about two common cultivars of C roseus which is named on the basis of their flower color that is the pink flowered Rosea and the

Comparison and Combination of Solvent Extraction and

Comparison and Combination of Solvent Extraction and

Comparison and Combination of Solvent Extraction and Adsorption for Crude Glycerol Enrichment Mali extraction with the non polar solvents a similar procedure was carried out except the non polar contaminant solvent phase was observed on the top and the glycerol rich phase was observed on the bottom The slow decantation was carried out and the enriched crude glycerol was obtained after

Colour Analysis Tools in ImageJ Auckland

Colour Analysis Tools in ImageJ Auckland

Work in combination Relates to RGB values CIE Lab Luminance L and two colour components a b which work in an opposing way Attempts to approximate human vision therefore has a larger colour gamut L 0 black L 100 white Biomedical Imaging Research Unit School of Medical Sciences Faculty of Medical and Health Sciences The University of Auckland Private Bag 92019 Auckland NZ

Autonomous Color Theme Extraction From Images Using Saliency

Autonomous Color Theme Extraction From Images Using Saliency

Autonomous Color Theme Extraction From Images Using Saliency Ali Jahaniana S V N Vishwanathanb and Jan P Allebacha aSchool of Electrical and Computer Engineering bDepartments of Computer Science and Statistics Purdue University West Lafayette IN 47907 U S A ABSTRACT Color theme palette is a collection of color swatches for representing or describing colors in a visual design or an

Oral Language Development in English language Learners

Oral Language Development in English language Learners

metaphors and quality of formal definitions and for cognates Inconsistent evidence for cross language relationships Phonological recoding Phonological short term memory Grammar little overlap in focus of studies